WAJUMBE CCM WABARIKI MABADILIKO MAKUBWA NDANI YA CHAMA CHAO

Wajumbe wa CCM wapitisha mabadiliko

Wajumbe 2,356 wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM leo wamepitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM kwa kauli moja chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli
Katika mkutano huo Rais Magufuli aliweka wazi lengo kuu la mabadiliko hayo ni pamoja na kuimarisha chama chao na kukufanya kiendelee kutawala na kufanya vyema siku hadi siku
“Mabadiliko yanalenga kuboresha mfumo na muunda wa chama chetu, wa sasa una mapungufu mengi utakuta watendaji wanafanya majukumu yanayofanana na kugongana kimaamuzi, pia kuliibuka vyeo vilivyo na nguvu, watu walivitumia kwa maslahi yao binafsi japokuwa kikatiba havipo”. Alisema Magufuli

Aidha Mwenyekiti huyo alitoa onyo kali kwa mamluki yeyote atakajitokeza kuharibu mchakato huo kwa namna moja ama nyingine na kusema adhabu kali dhidi yake itachukuliwa.

Kwa upande mwingine wajumbe wa mkutano huo wamekubaliana kuita ukumbi huo mpya jina la ‘Kikwete Hall’

“Leo tumekaa katika ukumbi huu mzuri kuna watu wamefanya kazi na miongoni mwao atakuwa ni Mzee wetu Jakaya Kikwete (Rais Mstaafu wa awamu ya nne). Mtakumbuka kabla ya hapa tulikuwa tukikaa kule yanatolewa magunia tunakaa,”Alisisitiza Magufuli

Makubaliano hayo yametokana na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dkt. John Magufuli kupendekeza kwa wajumbe hao ukumbi huo uitwe Kikwete kutokana na jitihada zake alizozifanya.
Previous Post Next Post