CHIRWA:NDOTO ZANGU ZA KUWA MFUNGAJI BORA ZITATIMIA

Bao aliloifunga Simba, limefufua matumaini ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa, kutaka kuwa mshindi wa tuzo ya mfungaji bora





Kitendo cha kuifungia timu yake bao la kusawazisha jana katika mchezo dhidi ya Simba kumetimiza malengo ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa, ambaye tangu atue kwenye timu hiyo hakuwahi kuwafunga wapinzani wao.

Chirwa ameiambia Goal, bao la jana analitoa kwa mashabiki wa timu hiyo ambao walifika kwa wingi kuwashangilia na kufanikiwa kusawazisha bao hilo baada ya Shiza Kichuya kutangulia kuwafunga.

"Kilicho nifurahisha ni bao ambalo nimeifunga Simba, kwasababu ndoto zangu siku zote tangu nije Tanzania ni kuifunga timu yenye upinzani na Yanga na siyo niyingine bali ni Simba, na kwakulifanikisha hilo nimeamua kutoa bao hilo kama zawadi kwa mashabiki wote wa Yanga," amesema Chirwa.


Mzambia huyo aliyefikisha mabao matatu hivisasa, amesema baada ya sare hiyo anaamini bado moto wa mabao ataendelea kuuwasha yeye na mshambuliaji mwenzake Ibrahim Ajibu ambaye kwasasayeye ndiyo kinara wa mabao kwenye klabu hiyo akiwa na mabao 5.

Mshambuliaji huyo ametamba kuwa malengo yake msimu huu, ni kuhakikisha anavuka kiwango cha mabao 12, aliyofunga msimu uliopita na ikiwezekana aweze kuibuka mfungaji bora na kutwaa tuzo ya mfungaji bora kwa mara yake ya kwanza.

SOURCE:GOAL.COM
Previous Post Next Post