Arsenal watenga donge nono kumbakisha Mesut Ozil
Klabu ya Arsenal ipo teyali kumtengea donge nono la mshahara Mesut Ozil
ikiwa ni ofa nono ya mshahara unaofikia paundi 280,000 kwa wiki ili
aweze kubakia katika klabu hiyo.
Kiungo huyo ambaye ni raia wa Ujerumani bado hajaamua kuhusu mustakabali
wake huku ikiwa imebaki miezi 15 katika mkataba wake wa sasa, na
kumekuwa na wasiwasi uliobuka kuwa anaweza kuondoka msimu huu wa
kiangazi.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal akikunja kitita cha paundi 140,000 kwa wiki ambazo zinaongezeka mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki huku akiongeza na bakshishi.
Arsenal wako tayari kumuongeza zaidi lakini Ozil anaonekana kama bado hayupo tayari akifahamu kuwa anaweza kupata zaidi akienda kwingine.