Kocha msaidizi wa Young Africans Juma Mwambusi amesema bado
hawajamaliza kazi ya mapambano ya mchezo huo wa hatua za awali, hivyo
watahakikisha wachezaji wanapata muda mzuri wa kujiandaa kabla ya
kushuka dimbani mwishoni mwa juma hili.
“Mechi hazijaisha, katika michuano ya champions league kuna mechi mbili na tumecheza mechi moja bado mechi moja hapa nyumbani,” – Juma Mwambusi.
“Kikubwa ni kujipanga kuhakikisha tunafanya vizuri nyumbani ili tuweze kuvuka hatua moja tutafute hatua nyingine.”
“Wachezaji wetu wako sawa ila Haruna anamaumivu kidogo, anahisi ana malaria lakini daktari atachukua vipimo kwa ajili ya kuhakikisha kwenye mechi yetu ya marudiano atakuwa sawa.”
“Sisi tumewafunga kwao wanaweza wakaja kwetu kivingine kwa hiyo, tunatakiwa tujiandae vizuri kuhakikisha hatupotezi uongozi wetu.”
“Wachezaji wao wazuri, wana wachezaji wawili kutoka Ivory Coast wametupa upinzani wa kutosha kikubwa ni mbinu ambazo tumekwenda nazo zimeweza kutupa matokeo ugenini.”
“Kikubwa ni kujiandaa kwa sababu hata wao walijiandaa ndio maana goli letu la kwanza tulifunga dakika ya 40 unaweza kuona ni timu ya aina gani lakini magoli mengine tulifunga kwa sababu walitupa nafasi baada ya kuanza kucheza mchezo wa wazi.

Tags:
MICHEZO