EMMANUEL OKWI AMTWISHA ZIGO LA LAWAMA MWAMUZI





Emmanuel Okwi, amesema bado anahasira na Yanga na baada ya kushindwa kuifunga kwenye mechi ya jumamosi atafanya hivyo duru la pili






Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi, amemlaumu mwamizi Elii Sasii, kwa kushindwa kumlinda kutokana na rafu alizokuwa akichezewa na mabeki wa timu ya Yanga

Okwi ameiambia Goal, mabeki wa Yanga, Kelvin Yondani na Endrew Vicent, walistaili kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na rafu za mara kwa mara walizokuwa wakimchezea kwenye mchezo huo.

"Nilimlalamikia mwamuzi mara kwa mara kumtaka awe makini na wachezaji wale lakini chakushangaza mwamuzi aliendelea kuwaangalia na kushindwa kutoa hata kadi ya njano kwa mmoja wao jambo ambalo liliwapa uhuru wa kuendelea kucheza ndivyo sivyo,"amesema Okwi.



Mshambuliaji huyo mwenye mabao nane hadi sasa amesema kwa kiwango alichokuwa nacho hadhani kama Yanga wanauwezo wa kuizuia Simba pindi wanapotaka jambo lao na sare ya jana ilitokana na msaada kutoka kwa mwamuzi huyo.

Amesema alikuwa na hamu ya kuifunga Yanga, jana lakini baada ya jana kushindikana anaiweka hamu yake na kusubiri mchezo wa marudiano ambao utachezwa mwakani na kutamba kuwa atahakikisha anawafunga


SOURCE:GOAL.COM
Previous Post Next Post